Niligutushwa toka usingizini jogoo alipowika kuashiria kwamba kumepambazuka. Ukweli usemwe sikutaka kuamka kutokana na vile nilivyokatiziwa ndoto kighafla. Kufumbuka kwa macho yangu aidha kulinidhibitishia peupe fedheha niliyonayo kando na ulimwengu wakheri niliokuwa usingizini; Kitanda kilikuwa ni kile kile chenye matendeguu legevu. Blanketi nayo ni ile ile yenye mashimo kadhaa; ndoto tu ndiyo iliyokuwa tofauti kwa maana kheri na fanaka tele.
Ijapokuwa sikupendelea nilivyoamshwa ilinibidi kujikwamua na kujitayarisha kwenda chuoni ambamo mda wa kufika humo ulikuwa unaniyoyomea haraka. Niliharakisha kuvaa sare zile zile za shule zilizochanika na kunywa staftahi iliyokuwa na ladhaa tofauti na ile niliyozoea. Kuitupia macho ya darubini ili kubaini hususan ni wapi palipoenda mrama, maziwa yalikuwa ni yale yale tu, majani chai vivyo hivyo mapishi ndiyo kidogo yalikuwa tofauti kwani hayakujumuisha sukari. Baada ya funda kadhaa kikombe changu kilikuwa bure, nikaokota mfuko wangu ulikokatikiwa kamba pande moja na kuondoka kwenda chuoni mwendo ukiwa ni ule ule wa…
View original post 586 more words